Wakazi wa
Mtaa wa Migombani, Uliopo Katika kata ya Segerea Manispaa ya Ilala
Jijini Dar Es Salaam wakiwa wamelizunguka gari la Afisa Mtendaji wa Kata
ya Segerea aliyefika majira ya saa tisa kamili mchana huu na kutangaza
kusitisha uchaguzi wa serikali ya mitaa kimya kimya.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa
kawekwa mtukati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila
sababu ya msingi. waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa segerea wakimuhoji
afisa mtendaji huyo sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati
hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo
cha kupigia kura cha Migombani.
Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea
Msimamizi
wa Uchaguzi wa serikali ya Mtaa wa Migombani katika Kituo cha uchaguzi
wa Migomabni akielezea sababu za kusimamisha uchaguzi huo kwa muda
kutokana na kusubilia barua ya kumtaka kuendelea na uchaguzi kutoka kwa
afisa mtendaji wa Kata ya Segerea aliyetaka kujaribu kusitisha Uchaguzi
huo kwa kisingizio cha Kutumwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Segerea, Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi
unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo
kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi
huo.Pembeni ni wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa
mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.
Hii ndio
barua aliyokuwa akiandika afisa mtendaji wa kata ya segerea inavyosomeka
ambapo baadae alienda nayo ofisi kwa kuongozana na wakazi wa migombani
kwaajili ya kugonga muhuri wa kata kuthibitisha kuwa uchaguzi unaendelea
Afisa
mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi
wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya
afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila
sababu za msingi
Wakazi wa
Mtaa wa migombani, Kata ya Segerea wakimzuia Afisa mtendaji huyo
kuondoka mpaka atangaze tena kuwa uchaguzi unaendelea.Picha na Josephat
Lukaza wa Lukaza Blog
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
Hali ya
Kushtusha imetokea katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani Mara
baada ya Afisa Mtendaji huyo kuja na kutangaza kimyakimya Kuwa UChaguzi
huo umesitishwa, Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kusikia
ndipo walipoanza sasa kutafuta mchawi na kumtia nguvuni afisa mtendaji
huyo wa mtaa kwa kutaka kujua sababu za msingi zinazopelekea yeye kuja
kutangaza kusitisha uchaguzi huo.
Afisa
mtendaji huyo baada ya kuulizwa sababu za msingi alijitetea kuwa
ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya ilala. Mara baada ya
Kutoa sababu hiyo ndipo wakazi wa mtaa wa migombani walipoona kuna
dalili za kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo walipomuweka mtu kati na
kumtaka Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa maandishi kuwa uchaguzi
unaendelea ndipo wakazi hao walipomuweka mtu kati na kuhakikisha
anaandika barua hiyo ya kutaka kuendelea na uchaguzi.
Mara baada
ya wakazi wa mtaa wa migombani kwenda nae katika ofisi ya kata kwaajili
ya kugonga muhuri kuthibitisha Uchaguzi huo kuendelea ndipo uchaguzi
ukaendelea na muda huu zoezi la kuhesabu kura linaendelea
إرسال تعليق