FBI yachunguza shambulizi la mtandao wa Twitter na You Tube

Akaunti ya Twitter na You Tube ni mojawapo ya mitandao iliyoshambuliwa na watiifu wa Islamic State.
Idara ya upelelezi ya Marekani-FBI inachunguza shambulizi la mtandao dhidi ya akaunti za Twitter na You Tube zinazomilikiwa na kitengo cha uongozi wa kijeshi cha Marekani ambacho kinafuatilia  mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani kwa kundi la Islamic State nchini Irak na Syria.
Washambuliaji ambao walisema ni wafuasi watiifu wa Islamic State  kwa muda mfupi walishambulia akaunti hizo siku ya jumatatu na kuwatishia wanajeshi wa Marekani kwa ujumbe unaosomeka “tunakuja, angalia nyuma. ISIS”.
Mtandao wa You Tube washambuliwa na ISISMtandao wa You Tube washambuliwa na ISIS
Jumbe nyingine zinajumuisha nyaraka kwenye tovuti ambazo zilikuwa zimeonekana zikiwa na namba za simu na dazeni za  anwani za barua pepe na anwani za majumbani mwa maafisa wa jeshi la Marekani.
Pia walionyesha kile kilichoonekana kuwa uvujaji wa ramani za kijeshi za China na Korea kaskazini.

Post a Comment

Previous Post Next Post