Dar es Salaam. Kuna baadhi ya mastaa wanaojua kuyatumia majina
yao, kwani licha ya kuwa mwigizaji na mtangazaji wa redio, Yvonne Cherry
‘Monalisa’ hafanyi kazi hizo pekee bali ana kampuni inayobeba tenda
mbalimbali katika sekta za umma na binafsi.
Monalisa aliliambia gazeti hili kuwa anapenda
kufanya mambo yake chinichini ndiyo maana walio wengi hawajui
anayoyafanya katika jamii.
Hata hivyo, alibainisha kuwa anafanya kazi katika
kampuni zaidi ya tatu kila siku na anatenga muda wa kuwa na familia
yake, hiyo ndiyo sababu pekee inayomwepusha kufanya mambo yasiyofaa.
“Mambo yangu huwa nafanya kimyakimya siyo lazima
upige makelele watu wakujue taratibu watu watakujua tu lazima, nina
kampuni yangu mwenyewe Sherry Company Limited na sasa hivi ni meneja wa
Manday Entertainment. Hii ni kampuni mpya wa filamu na burudani, tuna
studio za audio na video tunataka pia kuanza na usambazaji wa filamu,”
alisema.
Monalisa alisema kupitia kampuni yake ametengeneza
filamu nyingi. “Binti Nusa 1,2,3 nilitengeneza kupitia filamu yangu,
mara nyingi nafanya tenda mbalimbali ingawa sijajitangaza sana,” alisema
na kuongeza: “Inatengeneza vitu mbalimbali katika sekta za umma na
binafsi. Ukiachana na kampuni hizi mbili, nafanya kazi ya utangazaji na
pia tamthilia na filamu, niko bize kwa kweli.”
Kuhusu tasnia ya filamu, Monalisa alisema hakuna elimu ambayo haijatolewa kuhusu maisha ya kupendana kwa wanasanii.
“Tumeshahubiri umoja, watu tupendane kwangu mimi
naona hapa kila mtu afanye kwa nafasi yake ili tufikie mahala
tunapopataka,” alisema Monalisa na kuongeza: “Kuwa wasambazaji ni lazima
kuwa makini na masilahi ya msanii mmoja mmoja.
“Wasambazaji nao wanataka kulifanya soko letu liwe
gumu, nilikuwa kinyume na wao, namshukuru Mungu wizara ilishatoa tamko
kuhusu bei ya filamu iliyopangwa na kampuni ya kusambaza filamu ya Steps
kwamba isitishwe.
Filamu hazitauzwa tena Sh1,500, natumaini
wataendelea na msimamo wao huohuo na watakuja na bei elekezi ili sote
tufahamu kitakachokuwa kikiendelea.
Post a Comment