Hizi
ni dalili tosha za ubingwa. Mara nyingi timu bingwa pia huandamana na
bahati – bao la dakika ya 90 lililofungwa na Willian lilionyesha wazi
kuwa licha ya ubora wa timu yao, lakini Chelsea pia ina kismati.
Everton
waliojaribu kubana kwa kila hali, wakajikuta wanaachia dakika ya mwisho
ya mchezo na kuruhusu kikosi cha Jose Mourinho kiibuke na pointi tatu
muhimu.
Kwa
ushindi huo Chelsea inaendelea kuongoza kwa pointi saba safi kwenye
msimamo wa Ligi Kuu licha ya Manchester City nao kushinda 4-1 dhidi ya
Stoke City
Magoli
ya Manchster City iliyokuwa ugenini yalifungwa na Sergio Aguero (dakika
ya 33 na 70), James Milner dakika ya 55 na Samir Nasri (dakika ya 70),
wakati lile la Stoke lilifungwa dakika ya 38 na Peter Crouch.
إرسال تعليق