Baraza kuu la waamuzi limefungua mashitaka dhidi ya Craig Stephen ya mauaji ya wanafunzi watatu Waislamu.
Baraza
la waamuzi wa mahakama kuu nchini Marekani jana lilimfungulia mashitaka
rasmi mtuhumiwa wa mauaji ya wanafunzi watatu wa Kiislamu yaliyotokea
Kaskazini mwa Carolina nchini humo.
Baraza
la waamuzi wa mahakama ya jimbo la Durham lilimfungulia Craig Stephen
mashitaka ya kutisha kwa kutoa silaha hadharani na ya mauaji ya Deah
Barakat,23,Yusor Abu-Salha,21, na Razan Abu-Salha, 19 , kulingana na
WRAL tawi la CBS.
Mauaji
hayo yaliyotokea juma lililopita yalisababisha mmenyuko mkubwa katika
jamii ya waislamu Marekani na kote ulimwenguni, ikiongozwa na swali kuu
la kama chuki dhidi ya dini ndio iliyokuwa motisha ya mauaji hayo.
Hicks alikuwa jirani na wanafunzi hao na hapo awali, aliwahi kuhukumiwa mashitaka matatu ya shahada ya kwanza ya mauaji.
Uchunguzi
wa polisi umebainisha kuwa mauaji hayo yalisababishwa na 'mzozo juu ya
maegesho ya gari', lakini FBI pia imetangaza kuzindua uchunguzi tofauti
kama uhalifu wa chuki.
Deah
alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha North Carolina
kwenye kitivo cha Udaktari wa meno na Yusor ambaye alitegemea kuanza
masomo yake katika shule hiyo hiyo mwaka huu, walikuwa maharusi
wapya.Razan nae alikuwa ndugu yake Yusor na akisoma katika chuo hiko
pia.
Familia
ya waathirika wamelichukulia tukio hilo kuwa 'uhalifu wa chuki' moja
kwa moja, na Baraza la Uhusiano wa Uislamu-Marekani, shirika la haki za
kiraia la kiislamu, limeihusia serikali kuchunguza tukio hili bila
upendeleo wa aina yoyote.
Kurasa
ya Facebook kwa jina la Hicks ilibainisha chuki ya Hicks juu ya dini
kutokana na alivyojitambulisha kama asiye na dini 'mpenda silaha' na
maoni yake dhidi ya dini
إرسال تعليق