OYA MASELA, KAMA STAREHE ZINAUA SUMU YA NINI?

Niaje joo…inakuwagaje machalii wa kona mbaya kwa fasi ya kitaa. Kwa pande ya huku ni msupa hatare masela wangu. Hopu mko poa tangu lasti wiki nilipowasanua dheni nikabonyea kwenye mbishe za kusaka doo. Ama nini? Basi barida!
Kama vipi welikamu kwa jamvini tuanze kusebenza na mastori moo ya kitaa kama kawa kama dawa.
Bifoo sijazama kwenye kitu na boksi tupige kimya kwa sekunde bee kisha wote tuseme R.I.P kwa mzazi jembe Mjeda Komba kwa kutangulia mbele ya haki dheni kila kichwa kijue kwamba sote tupo rodi moko so ni masti kujiandaa kwa kujiweka klozi na Saa Godi. Hakuwa minsi nyingine kozi yeye ndo ananyaka kila kitu juu ya laifu letu kwenye feisi hii ya dunia.
Sori kibao ziifikie famili yake na watu wote wa nguvu ambao wameguswa katika wani wei au nyingine.
Ebana baada ya kujikumbusha maumivu kiaina ni taimu sasa ya kuzama kwenye mastori yetu tucheki kama yaliyomo yamo au magumashi?
Mazee laifu linaenda resi kinoma na huwezi kubilivu huu mwaka ambao juzikati tuliokuwa tunauona nyiu brandi tayari umeshaanza kuchakaa. Kama bado hujasomeka jipange mzazi.
Huku na huku kaka mkubwa nipo kitaa nakula misele pande za Tegeta kwa fasi ya Bongo tambarare.
Si ndo mwanangu mmoko akanipiga chabo dheni akataka kushea na mimi baba la baba juu ya mai waifu wake anavyomzingua kisa tu jamaa alikuwa akifanyiwa mambo f’lani saluni. Si unajua yale mambo ya masaji, maskrabu na mafasho?
Siyo sekreti, msela wangu anafunguka kuwa mai waifu wake ana majilazi hatare bati taimu hii ni noma zaidi.Ilikuwa lasti wikiendi. Kachaa katoka zake kwenye mbishe za kusaka bingo akiwa na mama la mama yaani maza wa makidi wake.
Kufika kitaa f’lani siti senta, kaka mkubwa akapaki ndinga dheni akamteli waifu kuwa amsikilizie ili anyoe kujiweka sopusopu kimtindo.Kweli waifu alikuwa mpole akachili kwenye mkoko akiendelea kula guudi miyuziki na kuchati si unajua tena mambo ya insta na whasapu?
Kachaa anakuteli kuwa baada ya kushevu kama kawa akajitupia kwenye kichumba f’lani ambacho hutumiwa kuoshea nywele au huduma nyingine. Jamaa anaamplifai kwamba shori mkare aliyekuwa anamuosha nywele alikuwa amepiga kitu cha jeki hapo kifuani so ilikuwa ni kwere tupu yaani ni shigidi sheeedah! Msela akawa anajiuliza sasa kama starehe zinaua, kuna sababu gani ya mtu kunywa sumu? Akaona kama mbwai…mbwai tu!
Basi baba la baba wakati akifanyiwa mandingo si ndo waifu akaibuka na kukuta kibanda kinataka kuungua faya?Mazee jamaa anakuteli kuwa waifu alimaindi kinoma maana aliona kila kitu laivu bila chenga. Kaka mkubwa alikuwa akifanyiwa mandingo yaliyompagawisha hatare! Unaambiwa weka mbali na makidi.
Unaambiwa baada ya pale waifu alibonyea akiwa amefura kinoma mzazi. Unajua alichokifanya?
Kachaa baada ya kumaliza sevisi alichomoka kwa mbwembwe zote. He! Kufika auti alipigwa na sapraizi kukuta waifu kasepa na ndinga.
Selaa akaona isiwe kitu. Akamvutia waya mama la mama ambaye alimtonya kuwa yupo kwa fasi ya homu na lazima siku hiyo kieleweke kudaadeki!Ebana msela kufika homu ndo kukaibuka bonge la mtiti hadi hapo tunapochili na mastori yetu bado hakijaeleweka. Waifu kanuna ileile ni mwendo wa mzungu wa nne.
Mmenisoma wana? Situwesheni haijatulia so ni beta kuchukua tahadhari kabla ya hatari.
Kama vipi sii yuu neksti wiki! Nduki!

Post a Comment

Previous Post Next Post