KATIKA
kile kinachoonekana kuwa ugomvi wao bado ni mbichi kabisa, nyota wa
filamu Bongo, Wema Sepetu Jumanne wiki hii akiwa ni mshehereshaji katika
sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtoto wa mtangazaji maarufu,
Zamaradi Mketema, aligoma kumtaja Kajala Masanja kama mmoja wa watu
waliotakiwa kula keki, Ijumaa lina mkanda kamili.
Nyota wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Kwenye sherehe hizo zilizofanyika nyumbani kwa mtangazaji huyo jijini
Dar, baada ya mambo mengi kufanyika, ndipo ulipofika wakati wa mastaa
kibao walioalikwa kuitwa majina yao kwa ajili ya kwenda kupewa keki
katika meza kuu.
Mshangao mkubwa ulikuja wakati Wema, akitangaza kwa mbwembwe
aliporuka kutaja jina la Kajala aliyekuwa akionekana dhahiri na kumtaja
aliyemfuatia, jambo ambalo lilizua minong’ono kutoka kwa waalikwa
wengine kiasi kwamba mmoja wao alichomoka na kwenda kumnong’oneza Wema
juu ya kitu hicho na kumtaka akirekebishe.
Nyota wa filamu Bongo, Kajala Masanja.
“Jamani mtaniudhi sasa hivi, mimi siwezi kumtaja huyo mtu mbona
mnanilazimisha nyie oooh,” Wema alisema kwa hasira kwa mtu huyo
aliyelazimika kuondoka zake ili kuepusha shari.
Mastaa hao waliokuwa wamekaa meza moja lakini kila mmoja akiwa bize
na mambo yake, waliwaumiza sana mastaa wenzao waliokuwa nao mezani kwani
wote wanawapenda lakini wenyewe ndiyo hawapendani.
Kuona hivyo, Kajala ambaye pia alichelewa kuingia ukumbini kabla ya
wenzake, aliamua kuondoka zake bila kusema chochote kuhusiana na suala
hilo lililoacha simulizi kubwa.
إرسال تعليق