WEMA KAMWAGA MBOGA, KAJALA AJIANDAA KUMWAGA UGALI

Staa katika tasnia ya Bongo Movie, Wema Isaac Sepetu.
Baada ya siku za hivi karibuni, Wema Sepetu kuamua kumwaga mboga kwa kumfungukia shosti wake wa zamani Kajala Masanja kwa kusema si rafiki mzuri na pia amefilisika, inadaiwa Kajala anajiandaa kumwaga ugali, Ijumaa limetonywa.
Rafiki wa karibu wa Kajala aliyeomba hifadhi ya jina lake, alimtonya mwandishi wetu kuwa maneno anayoyatoa Wema yanamkosesha amani mwenzake na kwamba siku si nyingi Kajala naye atajibu mapigo.
Kajala Masanja ‘Kay’.
“Si unajua wale wanajuana vizuri, walikuwa wanafichiana siri zao, alipofikia Wema akae mkao wa mambo yake kuanikwa, bado Kajala anatafuta ushauri wa namna ya kujibu mashambulizi, Wema kamwaga mboga, mwenzake atamwaga ugali,” kilinyetisha chanzo hicho.
Katika kujua ukweli wa ‘ubuyu’ huu, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Kajala kupitia namba yake ya mkononi lakini kila ilipopigwa haikupokelewa. Jitihada za kumtafuta zinaendelea ili ikiwezekana akimwaga ugali, Ijumaa liwe la kwanza kuripoti.

Post a Comment

Previous Post Next Post