Hii
ya leo inatokea Tandale Dar ni Hekaheka inayohusu binti anaedaiwa
kufungiwa ndani miaka 20 na bibi yake, watu wamehusisha tukio hilo na
imani za kishirikina, taarifa ikapelekwa Ustawi wa Jamii na Polisi.
Kaka
wa msichana huyo amesema mdogo wake ana matatizo ya akili, bibi yao
amekuwa mlezi wao baada ya wazazi wao kufariki.. anasema uamuzi wa
kumfungia dada yake huyo ndani ni kwa sababu ana nguvu sana na
wanapomuachia anafanya fujo ikiwemo kuharibu vitu na kuwapiga watu
Waianza kumfungia ndani baada ya babu yake kufariki, babu yake ndio alikuwa anakaa nae nje wakati akiwa hai.
Mjumbe
wa eneo hilo amesema ni kweli binti huyo ana matatizo na wanapomuachia
alikuwa anafanya fujo, wakaamua kumfungia kwa ajili ya usalama.. Mjumbe
anasema suala hilo hata ustawi wa jamii Magomeni wanajua, huyo bibi sio
mchawi kama watu wanavyodai.
Baadae
Polisi waliamua kumchukua bibi huyo kwa usalama kutokana na watu kutaka
kumchoma moto, msichana huyo aliyekuwa amefungiwa amepelekwa Hospitali
ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu
Post a Comment