Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amekiri
kuwapo kwa changamoto ya ajira kutokana na taasisi nyingi kukosa nafasi
za ajira nchini.
Amesema suala la ajira linahitaji ufumbuzi wa hali ya juu ili
wahitimu mbali mbali wanaomaliza vyuo vikuu kunufaika na kuondokana na
umasikini, ikiwamo kushirikiana na sekta binafsi katika kukuza soko la
ajira.
Lowassa aliyasema hayo juzi wakati wa hafla ya sherehe ya kutumiza
miaka 60 ya Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Mkongoro Mahanga, yeye
akiwa ndiye mgeni rasmi.
Lowassa alitoa wito kwa wazazi nchini kuwekeza kwenye elimu kwa
watoto na vijana wao ili taifa liliweze kuwa na wasomi wengi ambao
watakuja kuisaidia nchi kupata watalaamu kwenye nyanja mbalimbali.
Alisema kuwekeza kwenye elimu kwa watoto ni uwezekaji ambao utakuja
kusaidia familia kwa mambo mbalimbali ikiwemo ujasiliamali pamoja na
kupata viongozi walio bora wanaotegemewa na taifa.
Aidha, aliwataka vijana kuwa na malengo na kulipa kipaumbele suala
la elimu kwani ndiyo msingi imara hata kuwapata wanasiasa ambao
watalisaidia taifa hili kulipeleka mbele katika maendeleo.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo ni kuongeza shule za
awali hadi elimu ya juu ikiwa ni sehemu pekee ya kulisaidia taifa.
Kwa upande wake, Dk. Mahanga, amemhakikishia Waziri Mkuu huyo wa
zamani kuendelea kukabiliana na changamoto za ajira ikiwa ni pamoja na
kutatua matatizo ya ajira nchini na kutoa kipaumbele kwa vijana wa
kizalendo kadri ajira zinavyopatikana.
Alisena serikali itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi katika kukabiliana na changamoto za ajira.
Post a Comment