Abiria
zaidi 1000 waliokuwa wakisafari kutoka Musoma kwenda Dar es salaam
kupitia mikoa ya Mwanza na Shinyanga na wale wa kwenda mpakani mwa
Tanzania na Kenya Sirari pamoja na wa ndani ya mkoa wa Mara wameshindwa
kusafari baada ya madareva kuitisha mgomo.
Baadhi
ya madereva ambao wamekutwa katika kituo kikuu cha mabasi ya Bweri
mjini Musoma,wamesema kuwa mgomo huo umeitishwa kwa ajili ya kupinga
agizo la serikali la kukataa kusajili upya leseni zao hadi baada ya
kwenda kusoma katika vyuo vinavyotambulika serikalini.
Kwa
upande wao baadhi ya abiria wamesikitishwa na mgomo huo wa madereva
ambao umesababisha hata wagonjwa kushindwa kusafiri hivyo wameitaka
serikali kuchukua hatua za kumaliza migomo hiyo ambayo wamesema imekuwa
kero kubwa kwa wananchi.
Abiria
hao wameshuhudiwa wakiwa wamesimama kwa makundi katika kituo hicho
kikuu cha mabasi huku magari makubwa ya abiria yakishindwa kuingia
kabisa kituoni hapo hatua ambayo imesabisha baadhi ya abiria kulazimika
kukodisha magari madogo aina ya taxi kwenda jijini Mwanza kwa gharama ya
shilingi laki nne kutoka laki mbili za kawaida.
Post a Comment