Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini
(Tanesco), Felchesmi Mramba, amewahakikishia Watanzania kuwa hakuna
mgawo wa umeme.
Wakati Mramba akitangaza hakuna mgawo huo, baadhi ya maeneo
yamekuwa yakilalamika kukatiwa nishati hiyo bila taarifa yoyote ya
Tanesco.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
Mramba alisema Tanesco haijatangaza mgawo wa umeme na kwamba taarifa
iliyotolewa kwenye vyombo vya habari ni kuwapo kwa matengenezo ya kisima
cha Songas ambayo hufanyika kila mwaka.
Alisema mitambo hiyo imeanza kufanyiwa matengenezo tangu Machi 6,
mwaka huu na Shirika lilihakikisha hakutakuwa na athari yoyote kwa
wananchi.
Hata hivyo, alisema Tanesco ina vyanzo vya umeme vya kujitosheleza
katika kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa wateja wake. Mramba
alisema hali ya umeme kwa hivi karibuni imeathiriwa na mvua zilizonyesha
kwa mfululizo na kusababisha madhara katika nguzo za umeme.
Alisema miundombinu ya umeme imeathirika zaidi kwa jijini la Dar es
Salaam kutokana na kuwa chakavu kwa kuwa imejengwa tangu miaka ya1980
bila kubadilishwa.
Aliongeza kuwa changamoto hiyo imewaletea madhara ingawa hakusema
hasara iliyopatikana na kueleza kuwa bado hawajaijumlisha. “Hakuna mgawo
wa chini chini wala wa juu juu tulihakikisha katika matengenezo ya
kisima hicho cha Songas hapatatokea athari yoyote,” alisema.
Aidha, alisema kuna mitambo mipya ya umeme ambayo inaendelea
kujengwa na kwamba mwishoni mwa mwaka huu kutakuwa na nishati nyingi
kutokana na kukamilika kwa vituo hivyo pamoja na miundombinu
إرسال تعليق