Dar/Mikoani. Baadhi ya wabunge wa Chadema
wanaotetea viti vyao wameibuka kidedea katika kura za maoni
zilizofanyika katika majimbo mbalimbali nchini jana.
Hao
ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliyejizolea
ushindi mnono wa kura 356 akiwaacha kwa mbali wapinzani wake, Joyce
Mashine aliyepata kura43 na Tito Mwanjale kura 18. Wengine waliokuwa
wakiwania kuteuliwa na chama hicho ni Lazaro Mwankemwa aliyepata kura
15, Christopher Nyenyembe (12) na Sishe Simbeye (6).
Mbunge
mwingine, aliyepata ushindi wa kishindo ni Highness Kiwia wa Ilemela
aliyejizolea kura 134 na aliyemfuatia alikuwa Gasper Mwanaliela ambaye
alipata kura 28.
Wabunge wengine, Joshua Nassari hakuwa
na mpinzani katika Jimbo la Arumeru Mashariki kama ilivyokuwa kwa David
Silinde katika Jimbo la Momba.
Tafrani Mbeya Mjini, Mbarali
Awali,
kulizuka tafrani iliyotokana na mgombea, Meshack Kapange kuenguliwa.
Mgombea huyo alipinga akidai kuwa hakutendewa haki na kwamba
kilichofanyika ni kumkingia kifua Sugu.
Hata hivyo,
Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigita alisema Kapange
alikwishavuliwa uanachama na suala la kuchukua fomu za kuomba ubunge
ilikuwa ni haki ya kila mmoja.
Kapange alisema atakata
rufaa kwa kuwa hakutendewa haki na wasimamizi wa mchakato huo...
“Nimempigia Katibu Mkuu wa Chadema (Dk Willibrod Slaa), akaniambia yuko
kwenye mkutano Mwanza, nitampigia kesho (leo) kumweleza kunyang’anywa
haki yangu,” alisema. Mzozo mwingine uliibuka Mjini Mbarali baada ya
Jidawaya Kazamoyo aliyepata kura 109 kulalamika kuwa ndiye mshindi na
kuzuka vurugu zilizosababisha Liberatus Mwang’ombe aliyeshinda kwa
tofauti ya kura moja kutolewa nje ya ukumbi akiwa chini ya ulinzi mkali.
Matokeo ya kura ya maoni Chadema
Segerea: Anatropia
Theonest (49), Kisheli Mchele 26 Masato Wasira (24), Baraka Sawema
(15), Habron Mwakagenda (6), Bakari Yusuph (2), Loyce Gibona (2), Amos
Maziku (0), Dominic Orembe (0), George Martin (0).
Lupa: Miraji Hussein amepata kura (65) na kuwashinda wenzake Njelu Kasaka (45) na Fillipo Mwakibinga (32).
Korogwe Mjini: Amani
Kimea amewashinda kwa mbali wenzake watano kwa kupata kura 56.
Aliyefuata ni Mwakolo Wynjones (26), Calistus Shekibaha (8), Steven
Kimea (4), Benson Mramba (1) na Grayson Kibwana (0).
Busega:
David Nicad (116), Buluba Mabelele (67), Revocatus Madundo (55), Modest
Masunga (4), Sajda Dotto (3), Mapambano Ochalo (2), Keneddy Lufulondama
(1), Adam Komanya (0), Lutandula Mabimbi (0) na Mhere Mwita (0).
Sikonge: Godfrey Ndaki (16), Moses Kaombwe (17), Dk Mmeta Yongolo (19), Mtemi Zombwe (70) na Hija Ramadhani 83.
Manyoni: Alute Emmanuel (171) na Thedey Meremeta (47)
Vwawa:
Fanuel Mkisi (136), Stephen Mwamengo (42), Solomon Kibona (22), Andrea
Bukuku (9), Fadhil Shombe (8), Bob Mwampashe (5) na Jonathan Mwashilindi
(5).
Ilemela: Highness Kiwia (134),
Gasper Mwanaliela (28), Bugumba Nsumba (20), Wema Dilala (17), Deus
Ng’hanyanga (15), Edwin Sarungi (13), Telexphone Masalu (8), Kageshiza
Mwendesha (7), Mayalo Kasili (3), Thobias Mogole (7), Magesa Masinde
(6), Damas Kimenyi (5), Habath Matalu (5), Greyson Wanzagi (13), Darius
Ngocho (5), Humphrey Mmanda (3), Malehe Sweta (3) na Frederick Mataja
(2).
Mbozi: Paschal Haonga (82), Fredy
Haonga (34), Sophia Mwabenga (18), Ambukusye Kabango (4), Eliud Kibona
(3), Anastazia Nzowa (2), Eliud Msongole (1), Seule Nzowa (1) na Zabron
Nzunda (1).
Ileje: Emmanuel Mbuba (98), Gwamaka Mbughi (66) na Emmanuel Msyani (37).
Tunduma: Frank Mwajoka (130), Victor Nkonjela (20) na Clemence Nyondo (15).
Momba: David Silinde hakuwa na mpinzani.
Babati Vijijini: Daniel Karenga (14), Esther Sarwatt (17), Herman Sanka (5), Leonard Mao (3), Salum Shawishi (8) na Lawrence Tara (288).
Arumeru Mashariki: Joshua Nassari amepita bila kupingwa.
Makambako: Olaph Mhema (72), Fred Kalonga (57) na Kheri Kisingile (0).
Kibaha Mjini: Michael Mtali (62), Henry Msokwa (38), Ishaka Mnembwe (31), Joachim Mahega (13), Bosco Mfundo (4) na Frank Mzoho (3).
Mbeya Mjini: Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ (356) Christopher Nyenyembe (12), Joyce Mashine (43),
Lazaro Mwankemwa 15, Tito Mwanjale (18) na Sishe Simbeye (6).
Mbarali: Liberatus Mwang’ombe (110), Jidawaya Kazamoyo (109), Tazan Ndingo (25), Grace Mboka (14) na Dickson Baragasi (9).
Post a Comment