Capital-One-Cup-1
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Michezo ya robo fainali ya kombe la Capital One la nchini Wingereza linaloshirikisha ligi za Daraja la kwanza, pili na timu zinazoshiriki ligi kuu ya Wingereza imekamilika kwa timu nne kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali.
Matokeo ya robo fainali ilikuwa hivi;
Everton 2 – 0 Middlesbrough
Manchester City 4 – 1 Hull City
Stoke City 2 – 0 Sheffield Wednesday
Southampton 1 – 6 Liverpool
Baada ya michezo hiyo, ratiba ya michezo ya nusu fainali ni kama ifuatavyo;
Everton – Manchester City
Stoke City – Liverpool
Michezo ya nusu fainali itachezwa Januari, 4 na marudiano itakuwa Januari, 25 mwakani