TAMKO LA ACT-WAZALENDO JUU YA YANAYOENDELEA BURUNDI

TAARIFA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KWA  VYOMBO VYA HABARI

JUU YA MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI BURUNDI
TANZANIA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI IKOMESHE MAUAJI NCHINI BURUNDI

CHAMA cha ACT-Wazalendo kinasikitishwa sana na maujai yanayoendelea nchini Burundi na hasa Mji Mkuu wa nchi hiyo Bujumbura. Hali hii ya mauaji imesababishwa kwa kiasi kikubwa na uamuzi wa Rais wa sasa wa nchi hiyo Ndugu Piere Nkurunzinza kuendelea kugombea na hatimaye kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo katika mazingira yanayodaiwa kuvunja demokrasia na utawala bora.

Tangu machafuko hayo ya nchini Burundi yaanze zaidi ya watu 100 wameshauawa kufikia wiki hii na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Aidha, wimbi la wakimbizi kutoka Burundi linarudi kwa kasi na wengi wao wakikimbilia nchini Tanzania.
Bahati mbaya sana mpaka sasa Jumuiya ya Kimataifa na hasa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Burundi ni mwanachama, haikuchukua hatua za maana za kuzuia kuchafuka kwa utawala wa kidemokrasia na utawala washeria nchini Burundi, na wala haichukui hatua stahiki kuzuia mauaji yanayoendelea.

Hii ni kinyume kabisa na Mkataba unaounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao unatoa kipaumbele cha juu kulinda uhai na haki zaraia katika Jumuiya hizo
Kutokana na hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi, na kwa kuzingatia nafasi ya kihistoria ya Tanzania katika kutafuta na kufanikisha Mkataba wa Amani nchini Burundi, na kwa kuzingatia na fasi yake katikaJ umuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika, sis ACT-Wazalendo tunaitaka serikali ya Tanzania, kwa hali kubwa ya dharura, ichukue hatua zifuatazo:

1.Iitake serikali ya Jamhuri ya Burundi kukomesha mara moja mauaji yanayoendelea nchini humo na kuwahakikishia raia wanchi hiyo usalama

2.Tanzania Iitake serikali ya Jamhuriya Burundi kuitisha mkutano wa wadau  wote wasiasa na utawala nchini humo ilikujadili mustakabali wa nchi hiyo kisiasa na kijamii, ikiwemo uwezekano wa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayosimamia Katiba ya Burundi kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia

3.Tanzania Itumie nafasi yake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuitaka Jumuiya hiyo kuzuia machafuko nchini Burundi na kuhakikisha kwamba utawala wademokrasia na utawala wa sheria unazingatiwa nchini humo

4.Chama cha ACT-Wazalendo kinasisitiza kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki itakosa uhali wa kuendelea kuwepo kwake kama itaendelea kuwa Jumuiya ya viongozi wa nchi zinazounda Jumuiya hiyo huku ikishindwa kusimamia haki za kuishi na haki za kiraia za wananchi wa Afrika Mashariki.

Imetolewa leo jumatano 16 Disemba 2015
Na VenanceMsebo
Katibu wa Kamati ya Mambo yaNje

ACT-Wazalendo

Post a Comment

Previous Post Next Post