FORBES AFRICA PERSON OF THE YEAR 2016: Rais MagufuliHadi muda wa saa tisa Alasiri ya leo Oktoba 26.2016 kwa masaa ya Afrika Mashariki, tayari Rais wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe Joseph Magufuli ameweza kufikisha jumla ya  asilimia ya kula 84 katika kuwania tuzo maalum ya Forbes.
Hata hivyo, kwa kura hizo ni hatua ya ushindi wa moja kwa moja kwani ameweza kuwaacha mbali washiriki wengine wanaowania tuzo hiyo ambayo imekuwa ikiwaniwa na watu mbalimbali katika Bara la Afrika hasa ambao wameweza kufanya mambo kwa jamii ikiwemo wafanyabishara wakubwa pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu na Marais wa Nchi wa Bara la Afrika.
Mbali na Rais Dk. Magufuli wengne wanaowania kinyang’anyiro hicho ni  pamoja na Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel le Roux, Thuli Madonsela, Ameenah Gurib na watu wa Rwanda.
Sherehe maalum za tuzo hiyo zinatarajiwa kufanyika katika Jiji la Nairobi Nchini Kenya hapo Novemba 17.2016  hivyo endapo Rais Magufuli atafanikiwa kushinda tuzo hiyo, basi Tanzania itakuwa imepata tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo kwani mwaka jana 2015, mshindi wa tuzo hiyo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’.
Nawe unaweza kupiga kura yako kwa kuingia  kwenye tovuti ya  poy2016.com ambapo baada ya kuingia hapo, unaweza kugusa jina la mtu ambaye unapendekeza ashinde tuzo na hapo kura itakuwa imehesabiwa (Hii ni kwa kila kifaa kimoja yaani simu ya mkononi ama kompyuta yako).
Rais Dk. Magufuli anatimiza mwaka mmoja tokea watanzania wapige kura katika uchaguzi Mkuu wa Urais 2015, Oktoba 25 na baadae kutangazwa kuwa mshindi na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Andrew Chale-dewjiblog
dsc_0543Kura alizonazo hadi sasa Rais Dk.Magufuli
dsc_0550Mshindi wa Forbes 2011
dsc_0552Mshindi wa Forbes 2013
dsc_0555Mshindi wa Forbes 2014
dsc_0557Mshindi wa Forbes 2015
dsc_0559 4-2Rais Magufuli anayeongoza hadi sasa katika kinyang’anyiro hicho cha Forbes 2016