DEREVA
teksi Hamis Seleman (18), mkazi wa Vingunguti jijini Dar
es Salaam, amekufa baada ya kuchomwa kisu kifuani na Ali
Kimodo, aliyemfumania akiwa na mpenzi wake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema tukio hilo
lilitokea usiku wa saa 9:00 wa kuamkia mwaka mpya, katika
eneo la Vingunguti mtaa wa Magenge, ambapo Seleman
alifumaniwa na msichana mmoja (jina tunalihifadhi), mwenye
umri wa miaka 15, mkazi wa Tabata.
Nzuki
alisema kuwa baada ya tukio hilo kutokea, Kimodo pamoja na
binti huyo walitoroka, hivyo polisi inaendelea na
upelelezi kwa ajili ya kuwapata watu hao.
Aliongeza
kuwa katika maeneo mengine ya mkoa huo, hali ilikuwa
shwari katika sherehe hizo za sikukuu ya Mwaka Mpya.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya
Kihenya alisema hali ilikuwa shwari katika eneo lake,
kuanzia Krismasi na Mwaka Mpya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alisema
katika eneo lake, pia hakukuwa na tukio lolote kubwa la
uhalifu na hali ilikuwa shwari.
Post a Comment