Habari Zinazoenea Za Collaboration Ya Ali Kiba Na Chris Brown Sio Za Kweli - Habari Kamili Zipo Hapa

Kama wewe ni mtumiaji au mtembeleaji wa mitandao ya kijamii [na sijui nani hatumii hii mitandao siku hizi kwa njia moja au nyingine] bila shaka leo umeona habari inayozunguka kuashiria kwamba jikoni inapikwa collabo kati ya msanii wa Tanzania Ali Kiba na yule wa Marekani, Chris Brown.
Nilipoziona habari hizi, binafsi nilifurahi kwani naamini kwenye mafanikio ya sanaa na wasanii wa kitanzania katika kufika mbali zaidi kwa minajili ya kuitangaza Tanzania, utamaduni wake [ikiwemo muziki,sanaa nk] na hata kuwatangaza watu wake. Kila mtu mwenye akili timamu bila shaka anawaombea na kuwatakia kila la kheri wasanii wetu waendelee kutaka kutimiza ndoto zao za kufika mbele zaidi. Isitoshe Ali Kiba aliwahi kufika anga za mbali kiasi cha kushirikiana na artists wengine wakubwa barani Afrika na hata Marekani. Bila shaka unakumbuka project ya One8 iliyomkutanisha Ali na mkongwe wa R&B R.Kelly.
Lakini wakati naendelea kuisoma habari yenyewe, ghafla tabasamu langu likaanza kupungua kabla halijapotea kabisa. BBC Swahili? Mbona kwenye tovuti yao rasmi ya BBCSwahili.com habari hii siioni?  Tangu lini BBC Swahili wakatumia “blog”? Na mbona mengi yanayoelezewa hayaendani na kile ninachokifahamu? Tangu lini Ali Kiba yupo chini ya Samsung? Mbona VIP Beats ni wauzaji wa beats na sio watu wa habari? Kweli BBC wawe na site ambayo ina posts 2 tu? Mmmh
Nikaona nijiridhishe kwa kuwasiliana na uongozi au management ya Ali Kiba. Ndipo nilipoupata UKWELI kwamba habari hiyo haina ukweli hata kidogo na kwamba hakuna kitu kama hicho kwa hivi sasa. Naam. Tuendelee. Hili si la kweli! [Ila kama nilivyosema hapo juu, lingekuwa la kweli…sote tungelifurahia au sio?]

1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post