Ikiwa
Leo ni Siku ya kumbukumbu ya Kifo cha Hayati Sheikh Amri Abeid Karume
Muasisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba na Mmmoja wa Waasisi wa
Taifa La Tanzania Siku ambayo imekuwa Sambamba na Kumbukumbu ya Kifo cha
Marehemu Steven Kanumba aliyekuwa Muigizaji Nchini Tanzania Kala
Jeremiah @kalajeremiah ameamua Kufunguka Mengi Kuhusu watu hawa Wawili.
Akizungumza
na @DjHaazu Kupitia Kipindi Cha DUNDO LA MAMBO JAMBO RADIO, Kala
Jeremiah amemzungumzia Hayati Karume kama Mwanamapinduzi aliyewahi
Kutokea na Kuikomboa Zanziba na Kutokana na Hekima zake alizokuwa
amejaaliwa na Mungu aliona umuhimu wa Kuwapigania Wazanzibari wenzake
kwa kupigana Vita na unyanyasaji na Utawala wa Kimwinyi ulikuwepo
Zanzibar. Amesema Watanzania kwa Ujumla Tuitumie siku hii kwa Vitendo
kwa Kupinga Manyanyaso yote na ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya
Viongozi wa Serikali ya Jamuhuri ya TZ ikiwa ni pamoja na Kujitokeza
katika Kujiandikisha na Mwisho Kupiga Kura mwaka huu 2015 kwa ajili ya
kuchagua Viongozi WELEDI.
Hakuishia
Kumzingumzia Karume pekee bali amemzungumzia Pia aliyekuwa Nguli wa
BONGO MOVIE Steven ambaye naye alitutoka Siku kama ya Leo Mwaka 2012 kwa
kusema kuwa Kanumba alikuwa ni Msanii Mpambanaji aliyeipambania Sanaa
Ya Filamu Nchini Tanzania na Tokea Afariki Dunia Tasnia ya Filamu
Tanzania Imeyumba sana.
Kala Jeremiah anathamini sana Mchango wa Sheikh Karume na Mchango wa Steven Kanumba MSIKILIZE AKIZUNGUMZA KWA KU-CLICK LINK HII https://www.hulkshare.com/r9fdu8530lxc
Hayati Abeid Aman Karume
Hakika Itakumbukwa na Kuheshimiwa Historia Iliyoachwa na Hayati Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar ambaye Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi.
Karume aliongoza mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hapo mwaka 1964. Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa jina la Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hatosahaulika Pia Mpambanaji wa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania Steven Kanumba
Steven Charles Kanumba alizaliwa tarehe 8 Januari 1984, Shinyanga -na alifariki tarehe 7 Aprili 2012 alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania.
Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye
aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza
kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa
walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru
Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza
kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Post a Comment