OYA MWANA MDOLI FAMBA NDO UNAUZWA BEI GHALI!

Niaje…niaje wazazi majembe yangu? Inakuwa nini wanangu wenyewe? Kipande hii ni mpango mzima. Hapa ni mwendo wa kubandika na kubandua mwanzo mwisho. Ama nene? Mazee kitu cha Pasaka kilihapeni vipi? Dah! Siyo sekreti wana mlinifungia vioo bati haina kwere hopu mambo yalikwenda flenga. Basi barida!
Ebana eeh…tudei noo kumbwela dheni tunazama kwenye mastori moo fasta tuone kama yaliyomo yamo? Shujaa wangu mmoko kakutana na mzinguo hatare kinomanoma mazee. Tulia wewe upate hizi ni tamu ileile kudaadeki!
Jamaa bana anakwenda kwa jina la P. Baada ya kupiga kitu cha klasi vya kutosha dheni alipata promosheni ya kwenda kupiga mbishe za jobu kwenye mkoa f’lani hivi ameizing…kozi ni mkoa wenye laifu tamu kama mfukoni uko poa na kweli unapenda mambo ya madevelopumenti.
Basi kaka mkubwa akawa ni kibosile kwenye kampuni moko la ishu za kilimo kwanza.
Selaa akawa anapiga bakora si unajua zile za kiswazi? Pipo wakawa wanampiga chabo tu na swaga zake za mkwara mbuzi watu wanamcheki tu!
Ebana jamaa akiwa anamingo kitu cha mkoa si ndo akakamata mtoto mkare kitu cha kutoka uswazi si unajua tena dhahabu mchangani?Dosari kwa yule mtoto mzuri pale kati ni kwamba alikuwa ameshindikana kozi amesharuka na mameni kibwena bila kujali masela wa kitaa na washuwa mahazibendi wa watu.
Basi msela wangu naye akaingia kwenye kumi na nane za shori akawa anajipoozea kwa kula tu wepesi. Jamaa akawa anahudumia kinoma. Mara kumpiga usopusopu, bata ndefu na ishu zingine za dizaini hiyo.
Miezi bee tayari mtoto kashiba kitumbo ndii…hihaaa! Hapo ndo mchongo ulipomharibikia mwana kozi aliitwa na maparenti wa shori dheni akasainishwa ili ahudumie!
Dah! Huwezi amini msela akajikuta akishikishwa zigo ambalo hakupanga kuwa naye kwenye laifu. Wana wanakwambia ndo hivyo mdoli famba ndo huwa unauzwa bei ghali kinoma arifu.Miezi bee baadaye si msela akatakiwa kurudi makao makuu Bongo tambarare? Unaambiwa maparenti wa shori wakaweka kikao cha dharura kuweka ishu pleini.
Walichokuwa wanakompleini maparenti kwamba inawezekana kachaa akichomoka asirejee tena hivyo wataumbuka.Walichokifanya maparenti wakamfungashia shori akatimua na mwana. Msela alijaribu kufanya kila minsi ili kukwepa soo bati likamganda na sasa yupo na zigo bila kujiandaa.
Wana mmepata pointi? Samutaim ni beta kujipanga na siyo kwenda resi bila kufokasi mbele kujua fyucha itakuwaje? Cheki nawu mwana kapewa zigo ambalo hakuwa na taimu nalo tena kapewa na makosti kibwena.
Washikaji mmenisoma? Kama vipi kitu cha wikiendi hichooo…basi sii yuu neksti wiki mazee

Post a Comment

Previous Post Next Post